Friday 16 December 2016

Maisha Yetu Ni Kioo Cha Matendo Yetu.

Siku moja baba na mwanae walikuwa wakitembea milimani. Gafla mtoto yule alianguka, akaumia na kuangua kilio: 'AAAhhhhhhhhhhhhhhh!!!'
Alishangaa kusikia sauti ikijirudia mahala Fulani mlimani; ' AAAhhhhhhhhhh!!!!'
Akauliza kwa mshangao: 'wewe ni nani?'
Akajibiwa: 'wewe ni nani?'.
Kwa hasira akasema: 'mpuuzi'.
Akajibiwa:'mpuuzi'.
Akamtazama baba yake usoni na kumuuliza: ' Nini kinaendelea'.
Baba yake alitabasamu na kumwambia ' Fatilia kwa umakini'.
Mtoto akageukia tena mlima na kusema: ' nakupenda'.
Sauti ikajibu: 'nakupenda'.
Kijana huyu  akasema tena ' wewe ni mshindi '.
Sauti ikanguruma: 'wewe ni mshindi!' Kijana akashangaa lakini hakuelewa.
Ndipo baba yake alipoamua kusema: ' watu wanakiita kitu hicho mwangi, lakini ndiyo maisha halisi. Yanakurudishia kila kitu unachosema na kufanya. Maisha yetu ni kioo cha matendo yetu. Maisha yatakurudishia kila Mara kile kitu unachoyapa'.

Maisha yako sio kitu tu cha kuzaania. Ni mwangaza wako. Profesa Jay aliwahi kusema ' maisha kama kioo ukiyachekea nayo yanacheka'. Ukitaka kumjua mtu anayesababisha matatizo yako makubwa, angalia kwenye kioo. Ukimjua mtu anayesababisha matatizo yako makubwa hutabaki umekaa chini bila kufanya lolote kwa muda wa wiki tatu kama wewe ni mtu makini.
Mwanamuziki Stewart Johnson aliwahi kusema;

' Biashara yetu kwenye maisha sio kuwa mbele ya wenzetu, lakini ni kuwa mbele yetu sisi wenyewe, kuvunja rekodi zetu na kufanya kazi kabla ya ilivokuwa kabla '

Raph Waldo Emerson naye alikuwa na haya ya kusema ' Haiwezekani kwa mtu yeyote kudanganywa na mtu mwingine zaidi ya yeye mwenyewe'. Mtu unavyojidhania ndivyo unavyokuwa. Tusitengeneze vizuizi katika fikra zetu. Acha kuangalia pale tu chini ulipo an galia na juu unapoweza kuwa. Kuwa mwangalifu mawazo yako yanapokupeleka, maneno na matendo yako na uyafuate. Hakuna hatakayekushinda labda hujishindwe mwenyewe.

Unaibeba dunia mbayo kwayo inakubidi uishi ndani yake. Jua ya kwamba: ukiwa na ndoto kubwa, ubongo/kichwa chako kitakuwa Mali kubwa sana kwako. Je unavizuizi vingi katika maisha yako?. Mwanafalsa James Allen anakujibu ' wewe ni  kilema unayepaswa kumtazama. Ni wewe pekee unayepaswa kuchagua sehemu yako'. Kumbuka: kumbuka wewe ni daktari pekee unapopatwa na baridi, unapoisi kichwa kizito na unapokuwa na linapokuja swala zima la mtazamo.
   Frank Tyger anasema ' Maisha yako yajayo kwa asilimia kubwa yanategemea vitu vingi, lakini kwa asilimia kubwa ni wewe'. Unaweza kufanikiwa kama hakuna hata mtu mmoja anayekuamini, lakini huwezi fanikiwa kama hujiamini. Muongeaji maarufu na mwandishi  Zig Ziglar anasema ' Picha unayoiweka kichwani mwako utaifanyia kazi na kuifanikisha'. Ukibadilisha picha yako moja kwa moja unabadilisha na utendaji wako. Kila unachokiweka kwenye neno " mimi  ni " moja kwa moja unakuwa. Ukisema Mimi ni msomi utakuwa msomi. Mimi ni mkulimwa bora utakuwa mkulima bora. Ukisema mimi ni tajiri utakuwa tajiri. Ukisema mimi ni maskini utakuwa masikini. Ukisema naweza jambo Fulani utaweza . ukisema mimi siwezi hiki hutaweza.

Ni mimi rafiki na ndugu yenu.
Eddy Bide
Tuwasiliane:
0764145476
Whatsapp; 0625951842 (tuma neno "SUBSCRIBE " niwe nakutumia makala zangu)
Instagram; @eddybide

Endelea kuelimika kupitia blog hii. Asante

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: