Thursday 8 December 2016

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba Leo ni siku njema sana kwako. Siku yenye Baraka na tunu za kila heri. Nikushukuru pia kwa kuwa msomaji mzuri wa makala  zangu.

Karibu katika mada ya Leo inayosema:

Wewe Ni Nani?.
Jiulize swali umeumbwa duniani ili ufanye nini. Sisi sio tunda la ovyo la uumbaji wa Mungu. Mungu ametuumba ili tuongeze kitu katika kile kitu kinachoitwa maisha.

Wakati tunapozaliwa tunalia wakati dunia inafurahi ulishawahi kujiuliza kuhusu jambo hilo. Wewe unalia wengine wanafurahi. Kumbe kuna kitu ambacho tunabidi kuleta katika maisha aya ambayo Mungu ametuzawadia. Inakupasa Ujitahihidi katika maisha yako yote kile kitu kilichotokea wakati unazaliwa kitokee kinyume chake yaani unapofika muda wa wewe kufa ufe na furaha wakati ukiacha dunia katika majonzi na machozi mazito.

Kitu nilichijifunza katika maisha yangu ni kwamba usipochangamkia maisha, maisha yenyewe yatakuchangamkia. Siku zinakimbia na kuwa wiki, wiki zinakuwa miezi, miezi inakuwa mwaka. Usipofanya kitu chochote utabaki mtu mwenye manunguniko na majuto katika maisha yako. Bernard Shaw alipokuwa kitandani akisubiri kufa aliulizwa "ungefanya nini kama ungeweza kuishi maisha yako tena?"  Alijibu kwa sauti ya chini na yakupumua bila nguvu na kithembe akisema " ningependa kuwa mtu ambaye sikuwahi kuwa" nimeandika makala hii kwamba hiki kilichomtokea Bernard kisikutokee wewe.

Mungu aumbi mtumba Mungu aumbi vitu feki au vya kichina. Anaumba kitu kwa ufasaha kabisa. Utajiuliza ntawezaje kuishi maisha haya na kuyafurahia bila kuchelewa?. Jibu ni kwamba tafuta kichwani mwako umeumbwa kufanya nini. Umiza kichwa. Naamini kwamba kila mtu anakitu ambacho ni cha kipekee. Tupo humu duniani kwa hicho kitu cha kipekee. Kutafuta kipaji au kitu chako cha kipekee sio kwamba uache kitu unachokifanya kama kazi hapana. Namaanisha kwamba lazima ulete zaidi katika iyo kazi yako na kujikita katika mambo unayopenda kuyafanya. Inamaana hautiji watu wengine walete mabadiliko unayoitaji kuwa wewe wa kwanza kubadilika. Mahatma Gandhi aliwahi kusema "kuwa mabadiliko unayotaka kuyaona aswa katika dunia yako" na maisha yako yatabadilika.

Kahawa haikujua kwamba inaradha nzuri kabla haijakutana na sukari na maziwa. Wewe ulivyo mzuri unakuwa mzuri zaidi unapojiunganisha na watu wengine. Dunia imejaa watu wazuri/sahii (right people). Ukiwakosa inakubidi wewe uwe mtu sahii. Utajiri mkubwa ni hekima. Siraha kubwa ni uvumilivu. Mlinzi mkubwa ni imani. Kiungo kikubwa ni furaha. Msukumo mkubwa ni upendo. Na uhakika mkubwa ni Mungu. La kushangaza haya yote yanapatikana Burr wala hayapatikani sokoni wala supermarket.

Ni Mimi rafiki na ndugu yenu
Edius katamugora
Email;ekatamugora@gmail.com
0764145476
Whatsapp;0625951842
Www.bideism.blogspot.com

Endelea kusoma makala nzuri Kama hizi.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: