Tuesday 31 January 2017

Mungu Huwasaidia Wanaojisaidia

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na unaendelea vizuri kutimiza wajibu wako ili uendelee kusonga mbele.

Naomba nianze moja kwa moja kuongelea makala ya Leo "Mungu huwasaidia wanaojisaidia".. Mara nyingi watu wengi wamekuwa wakiongelea mafanikio lakini hawataji au kusema nguvu iliyopo nyuma ambayo ni ya uwezo wa Mungu(yeyote mwenye imani anaamini hivyo). Mungu ndiye aliyetuumba na ndiye anayetulinda usiku na mchana katupa pumzi na uhai na juu ya yote katupa uwezo wa kuvitawala viumbe vyote duniani. Asante Mungu.

Watu wengi waliofanikiwa huamini katika Mungu na wale wanao kwenda vinginevyo mafanikio yao huwa ni ya muda mfupi. Kumbe kuna kila haja ya kumuomba Mungu katika kila chochote kile tunachofanya.
Bofya

"Muombe Mungu ukiwa umeweka na nguvu zako" ni msemo wa kiafrika. Ndio maana nasema Mungu huwasaidia wanaojisaidia. Hata kama unasali namna gani kama ufanyi chochote juu ya kile unachokitaka unafanya kazi bure_,wahenga wanasema "unacheza ngoma kwenye maji" je unategemea itatoa sauti??.

Chukulia mwanafunzi ambaye hasomi lakini anasali sana, unategemea atafaulu?,hasha!. Au mkulima anayeacha shamba lake lishambuliwe na magugu na anasali sana ili apate mazao bora,unategemea apate mazao bora kweli?hukana lolote. Kuna msemo unasema "imani bila matendo imekufa" kumbe tukiwa na imani tuifanye katika vitendo ndipo Mungu naye atasikiliza maombi yetu.

Kuna hadithi moja inatufundisha juu ya jambo hili;
Katika mji mmoja kulitolewa tahadhari yakwamba siku za karibuni kutakuwa na mafuriko,watu wote wakaambiwa kuama kutoka sehemu zenye mabonde. Wote walioishi bondeni wakaama isipo kuwa bwana mmoja aliye sema "Bwana ataniokoa". Baada ya siku tatu mvua kubwa zikaanza,likaja gari aina ya jeep kumchukua,bwana yule akasema "bwana ataniokoa",gari lile likaondoka na kumuacha. Maji yakaendelea kuongezeka bwana yule akapanda juu ya paa la nyumba. Ikaja boti kumuokoa bwana yule akaendelea na msimamo wake wa kusema "Bwana ataniokoa". Maji yakaendelea kuongezeka bwana Huyo akaamua kupanda juu ya mti,helikpta ikaja kumuokoa bwana huyu akasema vilevile "Bwana ataniokoa". Maji yakaongezeka hadi yakamfikia shingoni akapaza sauti huku akiwa anatapatapa kwenye maji hayo mengi "Bwana nilikua na imani na wewe mbona ukuja kuniokoa?" Mungu akamjibu "Mpumbavu wewe, unazani jeep,helkopta na boti vilitumwa na nani?".

"Mungu huwasaidia wanaojisaidia"

"Imani bila matendo,imekufa".

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Tuwasiliane:
0764145476
0625951842 (Tuma neno "SUBSCRIBE" niwe nakutumia makala zangu moja kwa moja".
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram:@eddybide
Facebook page: bideismblog.

Usisite kuwashirikisha na wenzako kile ulichokipata. Asante.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: