Saturday 28 January 2017

Nidhamu Ni Ngao Kubwa Ya Mafanikio

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na unaendelea vizuri na michakato inayokupeleka kule unakokwenda. Nikushukuru kwa kuchukua wakati wako na kusoma makala hizi. Hakika umechagua kilicho bora.

Umewahi kujiuliza kwanini watu baadhi wanafanikiwa wengine hawafanikiwi?. Zipo sababu nyingi ambazo zinasababisha watu wengi wasifanikiwe. Leo hii nakuletea sababu moja muhimu ambayo itakufanya uingie katika Barabara ya mafanikio.

Nidhamu ni kitu muhimu sana katika mafanikio ya mtu yeyote. Ni ngao kubwa dhidi ya mafanikio. Kila mtu aliyefanikiwa  amebeba kitu kikubwa ndani yake ambacho ni nidhamu. Kila mahali panahitaji nidhamu,katika elimu,biashara,kazi na kila mahali.

Bofya hapa kusoma; Namna ya kutambua kipaji chako

Ukiwa mtu mwenye nidhamu utakuwa tayari kufanya kile ulichokifanya kwa moyo mmoja ata katika hali ngumu. Watu unaowaona leo wamefanikiwa wameweka nidhamu katika vitu vingi. Unahitaji nidhamu katika muda, unahitaji nidhamu katika matumizi ya fedha,unahitaji nidhamu katika kila kitu unachokifanya.

Nidhamu ni ngao dhidi ya changamoto mbalimbali itakupeleka tu kule unakokwenda. Ukiwa na heshima na nidhamu pia ni kisima cha Baraka, "waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani". Kumbe nidhamu imebeba kitu kikubwa ndani yake.

Bofya hapa kusoma: Hiki ndicho kiwanda unachokimiliki wewe

Kuna msemo wa kiswahili unasema "jiheshimu hueshimiwe" mtu mwenye nidhamu ni mtu anayejiheshimu pia na hivyo jamii inayomzunguka itampa heshima yake pia.

Wengi tumesikia hadithi ya sungura na Kobe.
Siku moja sungura na kobe waliitwa katika mashindano ya mbio. Mashindano yalianza kama ilivyo kuwa ada, sungura alikimbia kwa kasi sana na kupotea mbele za macho ya Kobe, alipofika njiani akaamua kupumzika akitambua kwamba Kobe anamwendo wa taratibu. Sungura huyu alipitiwa usingizi wa pono na kulala fofofo, kushutuka alikuta kobe kamaliza kuzunguka eneo la shindano na ametangazwa mshindi. Tujifunze nini katika hadithi hii?. Kuna watu wanauwezo wa kufanya maajabu makubwa lakini utovu wao wa nidhamu unawafanya waanguke kwenye kundi la sungura, wengine wanabaki wamejikita na nidhamu ya kile wanachokifanya (focus), mwisho wa siku wanafanikiwa. Kundi la sungura baadae ndio wanaokuja kufikiri yakwamba mafanikio ni bahati, hasha! Ni kwamba walikosa nidhamu kwa kile walichopaswa kufanya.

"Nidhamu ni ngao kubwa ya mafanikio"

"Jijengee nidhamu katika kile unachokifanya,utafanikiwa".

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora

Tuwasiliane:
0764145476
Whatsapp: 0625951842 (Tuma neno "SUBSCRIBE" niwe nakutumia makala zangu moja kwa moja).
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram: @eddybide

Facebook page: bideismblog (usisite kulike).

Washirikishe na wenzako kile unachokipata hapa. Asante.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: