Monday 8 March 2021

Edius Katamugora Afunguka Mazito Kuhusu Kitabu cha Jinsi ya Kuzifikia Ndoto Zako
 Asema Ni kitabu Bora Kuwahi Kuandikwa Kwenye Eneo Lake

Edius Katamugora ni mwandishi mbobevu akiwa ameandika vitabu kadhaa kwenye maendeleo binafsi. Amepata nafasi ya kusoma kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO na haya hapa ndiyo anayosema;

“Wakati ujao unamilikiwa na wale wanaoamini katika uzuri wa ndoto zao,” alisema Eleanor Rososevelt mke wa aliyewahi kuwa rais wa Marekani Franklin D. Roosevelt.

Je, wewe una ndoto na unaamini kwamba inaweza kuwa kweli? Kama ni kweli basi kitabu hiki kinakuhusu sana lakini kama wewe pia unazo ndoto lakini bado hauamini kama zinaweza kutimia basi kitabu hiki ni mwanga katika njia yenye giza nene.


Ndoto sio kile unachokiota wakati umelala bali ndoto ni kitu kinachokufanya ukose usingizi. Kwa msingi huo ukiendelea kulala sio rahisi kutimiza ndoto zako, bali ukiamka unaweza kuzifanya ndoto zako kuwa kweli.


Baada ya Mama Teresa kufanikiwa na kuwa maarufu kwa sababu aliwahudumia wagonjwa na watu waliokuwa wakifa katika mitaa ya Calcutta, India, watu ambao aliwahamasisha walimtafuta. Muda mwingi walisema, “Ooh Mama Teresa! Nataka kufanya unachokifanya” Nataka kuacha kila kitu ninachomiliki na kujiunga na kazi yako!” Muda wote alikuwa akiwajibu kwa maneno haya matatu, “Tafuta Calcutta yako.”


 Kwa lugha rahisi tunaweza kusema “Fuata ndoto yako” ni huyu huyu mama Teresa aliyesema, “Kama kila mmoja akisafisha uwanja wake dunia nzima itakuwa safi” kwa mantiki hiyo kama kila mtu akifanya jambo kuhusu ndoto yake dunia inaweza kuwa sehemu nzuri sana.


Binafsi naamini kwamba kila mtu anazo ndoto ambazo anatakiwa kuzifanyia kazi, mwandishi wa kitabu hiki ameandika kwa uzuri na ubora wa juu mbinu na namna mbali mbali za kuzifikia ndoto zako.


Wenye ndoto ni wale watu wanaosema maneno, “Liwalo na liwe” lazima nitimize ndoto zangu. Nilipokuwa natizama filamu ya kizungu iitwayo The Shawshank Redemption nilijifunza kitu kimoja kwamba ukiamua kufanya chochote unaweza kukifanya kikubwa ni kuweka nia na matumaini. Andy Dufresne ambaye aliweza kutoroka gerezani anasema, “Kuwa Bize Ukiishi au kuwa bize ukifa ” maneno haya yamewekwa wazi na mwandishi anapotukumbusha kwamba kuna kitu tunahitaji kufanya kwa ajili ya ndoto zetu, lazima siku tukiondoka tuniani tuache alama.


Mwandishi wa kitabu hiki amenitafakarisha sana aliposema, huwa tukifa wanasema, ร„pumzike kwa amani,” anaendelea kusema kwamba “Kuna watu hawasitaili kuambiwa ampumzike kwa amani maana muda wao mwingi hapa duniani ulikuwa wa kupumzika”.


Amka sasa usibweteke anza kuzifanyia kazi ndoto zako. Kumbuka kwamba watu wote waliofikia ndoto kubwa hawakuanzia pakubwa walianzia padogo. Kuna aliyewahi kusema, “Kinachoanzia juu ni kaburi tu”, hata kama vitu fulani havijakamilika wewe anza tu.


Kwenye safari ya kuifikia ndoto yako au kuzifikia ndoto zako lazima ukumbane na vigingi, lakini kumbuka hakuna ushindi bila mapambano lazima uyashiriki mapambano hayo.


 Kila hatua mpya inahitaji wewe mpya na mbinu mpya lazima uwe umejipanga.


Inawezekana umekua ukisaidia kutimiza ndoto za wengine, sasa ni wakati wako kuamka na kuanza kufanyia kazi ndoto zako, unaanzaje kuzifanyia kazi ndoto hizo, mwongozo ulio katika kitabu hiki ni dira tosha iliyosheheni madini na ramani ya kukupeleka kule unakotaka kufika na hata zaidi.


Nafikiri kitabu hiki ni kitabu bora zaidi kukisoma katika vitabu vya Kiswahili nilivyowahi kusoma kuhusu nama ya kuzifikia ndoto zangu, kimenijenga sana na nimepata vitu vingi vipya ambavyo kweli sikuvifahamu.


Mwandishi wa kitabu hiki, Godius Rweyongeza ni mtu ambaye nimemfahamu na kumfuatilia kwa muda mrefu, mambo mengi anayoyaandika ni yale ambayo tayari anayafanyia kazi na yameleta matokeo hivyo ukifuata kile alichoandika ndugu Godius hautaacha kufika mbali sana.


Nikusihi ukisome kitabu hiki si mara moja bali mara nyingi uwezavyo kwani madini yaliyo humu ni lulu tosha ya kukuvusha wewe katika hatua uliyopo na ukafika katika hatua zingine.


Pia maneno unayoyasoma humu yaweke katika matendo, kuwa na vitu vingi kichwani bila kuviweka katika matendo ni sawa na kuwasha gari bila kuliondoa, haufiki kokote. Ukitaka kufika mbali fanya kwa matendo.


Mwisho wa yote kumbuka, dunia inawapokea kwa mikono miwili wale wanaofanya mambo katika matendo na kwa ubora wa hali ya juu, kwa msingi huo naunga hoja ya Ralph Waldo Emerson aliyewahi kusema, “Kama mtu akiandika kitabu kizuri, akahubiri mahubiri mazuri, au akatengeneza mtego wa panya mzuri kuliko jirani yake, hata akijenga nyumba yake msituni, dunia nzima itatengeneza njia hadi mlangoni kwake.”


Utumie muda wako vizuri maana kila kitu ni zao la muda. Vitu vyote vizuri unavyoviona vilitengenezwa ndani ya muda fulani. Tumia muda wako kujiendeleza na kujifunza kuhusu mambo yanayohusu ndoto zako, tumia muda wako kwa wengine na mwisho tumia muda wako kutengeneza huduma au bidhaa fulani. Hivi ndivyo watu wote wenye ndoto kubwa walivyofanya na kufikia hatua za juu.


Nampongeza sana na tena sana ndugu Godius Rweyongeza kwa kitabu hiki kizuri kinachoelimisha, hamasisha, tafakarisha lakini pia kinaburudisha kupitia stori mbalimbali alizotuwekea humu.


 *Ukianza kusoma kitabu hiki hutokichoka!* 


Ndimi,

Edius Katamugora (Kijana wa Maarifa)

Mwandishi kitabu cha Yusufu Nina Ndoto. 



Rafiki yangu, bila shaka umeona aliyosema Edius Katamugora. Binafsi sima Cha kuongeza labda kukwambia tu kuwa sasa ni zamu yako kupata kitabu hiki. Nakala ngumu ya kitabu hiki ni elfu 20 tu. 


Ukiihitaji soft copy ya kitabu hiki pia inapatikana pamoja na vitabu vingine Viwili kwa elfu 19,999.

Karibu Sana. Tuwasiliane kwa 0755848391 karibu

Sunday 14 February 2021

ALICHOANDIKA Padre Dkt Faustin Kamugisha Mtunzi wa Kitabu Matatizo si Tatizo Kuhusu Kitabu cha YUSUFU NINA NDOTO

Mtunzi wa kitabu hiki ni mwandishi maarufu wa vitabu vya mafanikio. Ujumbe wa kutafakarisha na kusisimua wa kitabu hiki ni kuwa,  ukiwa na uwezo wa kuota ndoto bila kulala usingizi unakuwa na uwezo wa kubadili maisha yako. 

 



Ukibadili unachokiota unabadili unachokizalisha, unabadili maisha yako. Mfano wa kuigwa wa muota ndoto ni Yusufu wa Agano la Kale.  Ndoto yake ilizongwa na misukosuko. Ndugu zake waliomuonea wivu na kumuuza. Ndoto yake waliiwekea nukta, Mungu aliweka alama ya mkato. Mtunzi ameinakishi dhana ya ndoto kwa maneno ya kutia matumaini katika sura 39.                                                               

                             

Hata nyota ya ndoto yako ikipotea kama nyota ya Yusufu ilivyopotea ni MARUFUKU KUKATA TAMAA. Nyota ya ndoto itaonekana tena.  

Kuna mambo mengi ya kufanya kufanikisha  ndoto. Anza na ulichonacho na anzia ulipo. Ukitaka kutimiza ndoto zako lipa gharama za ndoto.  Amka kabla ya ndege wa angani kuzitekeleza ndoto zako.  Ili usipishane na ndoto zako hesabu baraka zako na si balaa. Ukiilinda afya yako, umeilinda ndoto yako.  Ukiwa na ndoto usipige kelele, watu wataona matokeo ya ndoto zako.  Tofautisha  ndoto zako na ndoto za watu wengine, kuwa wewe zaidi.  Ukiwa na ndoto ambatana na watu wenye ndoto. Kaa na waridi unukie. Ng'ang'ania ndoto yako kama stampu kwenye bahasha. 

                                    

Nampongeza ndugu Edius  Katamugora kwa kazi hii nzuri sana. Kitabu hiki Yusufu Nina Ndoto ni dira kwenye barabara ya mafanikio. Kisome hutajuta kwa nini umekinunua!

 (Padre Dkt Faustin Kamugisha Mtunzi wa Kitabu Matatizo si Tatizo).

Ili kupata kitabu hiki wasiliana na mwandishi Edius Katamugora kupitia namba 0764145476.

Kitabu kinapatikana kwa shilingi 12,000/= tu, kinafika mahali popote Tanzania. 

Thursday 4 February 2021

NI RAHISI! JIPATIE VITABU VYA UJASIRIAMALI (PDF) NDANI YA DAKIKA 5 (GET ENTREPRENEURSHIP BOOKS IN FIVE MINUTES)

 Sifa mojawapo ya mjasiriamali aliyefanikiwa ni kujijengea tabia ya kuwa mwanafunzi wa maisha yaani mtu anayejifunza mambo kila kukicha.

 


kama mjasiriamali pia unatakiwa kujijengea tabia ya kusoma vitabu mara nyingi uwezavyo. Les Brown mwandishi na mhamasishaji mashuhuri anasema ili uweze kuzifikia ndoto zako kwa haraka tengeneza utaratibu wa kusoma kurasa zisizopungua walau 30 kila kukicha.

Kitabu kimoja huwa na wastani wa kurasa 200 na vingine pungufu ya hapo. Ukijenga tabia ya kusoma kurasa 30 kila siku kwa mwaka mmoja utakua umesoma vitabu 52 na ziadi kwa miaka kumi utakuwa umesoma vitabu takribani 600.

                            

Kuna tofauti kubwa kati ya mjasiriamali anayesoma mara kwa mara na yule ambaye hana tabia ya kujisome au kujifunza vitu.

Je unatamani kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio na hujui ni vitabu gani usome vitakavyokusaidia kwenye kazi yako ya kijasiriamali?

Kama jibu ni ndiyo basi usiwaze kabisa maana shida yako imetatuliwa. Nimekuandalia vitabu 15 muhimu na zawadi ya kitabu kimoja vitabu hivi ni vya kingereza lakini hicho kimoja ni cha Kiswahili.

Kitabu cha Kiswahili kitakufundisha namna ya kukuza biashara yako kupitia intanenti au mtandao. Kumbuka nusu ya dunia sasa inatumia intaneti, unachelewa nini kuipeleka biashara yako mtandaoni na kuwa ya kimataifa? Je unahitaji kupanua biashara yako kupata wateja zaidi kitabu hiki kimebeba majibu yote.

 Ili upate vitabu hivyo 11 muhimu kwa kila mjasiriamali tuma neno "MJASIRIAMALI PACK" kwenda nambari 0764145476 kwa njia ya SMS kisha nitakutumia vitabu hivyo ndani ya dakika tano. Huduma hii inapatikana kwa bei ya ofa ya elfu tano tu (5,000/=) kwa watu 10 wa mwanzo kisha itakuwa elfu kumi (10,000/=) baada ya hapo.

 Wahi ofa hii ni ya muda mfupi tu, baada ya hapo kuna uwezekano mkubwa isipatikane.


Wednesday 6 May 2020

KITABU: PUMBA ZA EDIUS


Kitabu hiki ni kitabu chenye misemo ya hekima, mwandishi amekipa jina dogo la MAMBO MUHIMU TUNAYOYACHUKULIA POA MAISHANI. Waliosoma kitabu hiki wote wamekubali kwamba ni kitabu kinachopaswa kusomwa na kila mtu.


Kitabu hiki kinapatikana bure kabisa. Wasiliana na mwandishi 0764145476 ili uweze kukipata.

Edius Katamugora
0764145476

Sunday 3 May 2020

KITABU: NATAMANI KUANZA KUSOMA VITABU (Mwongozo wa kujenga Tabia ya Kusoma Vitabu)

Lipia 4000 na utatumiwa kitabu hiki ( WhatsApp au email) papo hapo. Kipo katika mfumo wa nakala laini (soft copy).

Kwa kiasi hicho kidogo utakachotoa  utajifunza yafuatayo:

1. Faida za kusoma Vitabu

2. Kwanini watu hawasomi vitabu

3. Namna ya Kujenga Tabia ya Kusoma Vitabu.

4. Kanuni ya 2 × 3 × Akili: Ukiifahamu kanuni hii hautawahi kuishiwa pesa mfukoni.

5. Tovuti zaidi ya 20 za kupata vitabu bure mtandaoni.

6. Orodha ya vitabu zaidi ya 100 unavyoweza kuanza navyo kuvisoma.



7. Namna ya kumjengea mtoto mdogo tabia ya kusoma vitabu.

8. Siri walizozificha matajiri kuhusu vitabu.

9. Siri walizoficha wanawake wanaosoma vitabu.

Haya yote utayapata kwa uchakavu wa shilingi 4000 tu.

๐Ÿ‘†๐Ÿพ๐Ÿ‘†๐ŸพLengo la kitabu hiki ni kuwafikia Watu 30000. Ili tufanye hivyo watu 50 wa kwanza kulipia 4000 watapata kitabu hichi haraka sana.

Mbali na kupata kitabu watu hao watakuwa wakielekezwa na mwandishi kwa muda wa mwezi mmoja namna wanavyoweza kujenga tabia hii.

Namba ya Malipo 0764145476 Jina Edius Katamugora. Ofa hii ni kwa muda maalumu na wakifika 50 itakwisha.

N.B: Kama hautaona mabadiliko ndani ya siku 90 bila 100% guaranteed.

Karibu ujipatie maarifa haya.

Ukishalipa tuma ujumbe ulioandikwa, "BOOK" utatumiwa kitabu mara moja.

Edius Katamugora
Author of 7 books
Content Creator
Creative Writter

KITABU: YUSUFU NINA NDOTO
KUHUSU KITABU


Mtunzi wa kitabu hiki ni mwandishi maarufu wa vitabu vya mafanikio. Ujumbe wa kutafakarisha na kusisimua wa kitabu hiki ni kuwa,  ukiwa na uwezo wa kuota ndoto bila kulala usingizi unakuwa na uwezo wa kubadili maisha yako. Ukibadili unachokiota unabadili unachokizalisha, unabadili maisha yako. Mfano wa kuigwa wa muota ndoto ni Yusufu wa Agano la Kale.  Ndoto yake ilizongwa na misukosuko. Ndugu zake waliomuonea wivu na kumuuza. Ndoto yake waliiwekea nukta, Mungu aliweka alama ya mkato. Mtunzi ameinakishi dhana ya ndoto kwa maneno ya kutia matumaini katika sura 39. Hata nyota ya ndoto yako ikipotea kama nyota ya Yusufu ilivyopotea ni MARUFUKU KUKATA TAMAA. Nyota ya ndoto itaonekana tena.  Kuna mambo mengi ya kufanya kufanikisha  ndoto. Anza na ulichonacho na anzia ulipo. Ukitaka kutimiza ndoto zako lipa gharama za ndoto.  Amka kabla ya ndege wa angani kuzitekeleza ndoto zako.  Ili usipishane na ndoto zako hesabu baraka zako na si balaa. Ukiilinda afya yako, umeilinda ndoto yako.  Ukiwa na ndoto usipige kelele, watu wataona matokeo ya ndoto zako.  Tofautisha  ndoto zako na ndoto za watu wengine, kuwa wewe zaidi.  Ukiwa na ndoto ambatana na watu wenye ndoto. Kaa na waridi unukie. Ng'ang'ania ndoto yako kama stampu kwenye bahasha. Nampongeza ndugu Edius  Katamugora kwa kazi hii nzuri sana. Kitabu hiki Yusufu Nina Ndoto ni dira kwenye barabara ya mafanikio. Kisome hutajuta kwa nini umekinunua! (Padre Dkt Faustin Kamugisha Mtunzi wa Kitabu Matatizo si Tatizo)

















Unaweza kupata kitabu hiki kwa mawakala wafuatao;

Mawakala wa kitabu cha YUSUFU NINA NDOTO

Arusha (DL BOOKSTORE -Sanawari) - 0787163013

Bukoba (Education Point -Kashai) - 0620690881
Dar es Salaam - 0753664083

Dodoma (Lugarawa Bookshop -Barabara 8) - 0685097713

Geita - 0743690673

Mbeya - 0764145476

Mwanza - 0782492069

Zanzibar - 
ABDUL 0713490778
 BAKAR 0774474208

ENEO MCHINA MWANZO ZANZIBAR