Asema Ni kitabu Bora Kuwahi Kuandikwa Kwenye Eneo Lake
Edius
Katamugora ni mwandishi mbobevu akiwa ameandika vitabu kadhaa kwenye
maendeleo binafsi. Amepata nafasi ya kusoma kitabu cha JINSI YA KUFIKIA
NDOTO ZAKO na haya hapa ndiyo anayosema;
“Wakati ujao
unamilikiwa na wale wanaoamini katika uzuri wa ndoto zao,” alisema
Eleanor Rososevelt mke wa aliyewahi kuwa rais wa Marekani Franklin D.
Roosevelt.
Je, wewe una ndoto na unaamini kwamba
inaweza kuwa kweli? Kama ni kweli basi kitabu hiki kinakuhusu sana
lakini kama wewe pia unazo ndoto lakini bado hauamini kama zinaweza
kutimia basi kitabu hiki ni mwanga katika njia yenye giza nene.
Ndoto
sio kile unachokiota wakati umelala bali ndoto ni kitu kinachokufanya
ukose usingizi. Kwa msingi huo ukiendelea kulala sio rahisi kutimiza
ndoto zako, bali ukiamka unaweza kuzifanya ndoto zako kuwa kweli.
Baada
ya Mama Teresa kufanikiwa na kuwa maarufu kwa sababu aliwahudumia
wagonjwa na watu waliokuwa wakifa katika mitaa ya Calcutta, India, watu
ambao aliwahamasisha walimtafuta. Muda mwingi walisema, “Ooh Mama
Teresa! Nataka kufanya unachokifanya” Nataka kuacha kila kitu
ninachomiliki na kujiunga na kazi yako!” Muda wote alikuwa akiwajibu kwa
maneno haya matatu, “Tafuta Calcutta yako.”
Kwa lugha
rahisi tunaweza kusema “Fuata ndoto yako” ni huyu huyu mama Teresa
aliyesema, “Kama kila mmoja akisafisha uwanja wake dunia nzima itakuwa
safi” kwa mantiki hiyo kama kila mtu akifanya jambo kuhusu ndoto yake
dunia inaweza kuwa sehemu nzuri sana.
Binafsi naamini
kwamba kila mtu anazo ndoto ambazo anatakiwa kuzifanyia kazi, mwandishi
wa kitabu hiki ameandika kwa uzuri na ubora wa juu mbinu na namna mbali
mbali za kuzifikia ndoto zako.
Wenye ndoto ni wale watu
wanaosema maneno, “Liwalo na liwe” lazima nitimize ndoto zangu.
Nilipokuwa natizama filamu ya kizungu iitwayo The Shawshank Redemption
nilijifunza kitu kimoja kwamba ukiamua kufanya chochote unaweza
kukifanya kikubwa ni kuweka nia na matumaini. Andy Dufresne ambaye
aliweza kutoroka gerezani anasema, “Kuwa Bize Ukiishi au kuwa bize ukifa
” maneno haya yamewekwa wazi na mwandishi anapotukumbusha kwamba kuna
kitu tunahitaji kufanya kwa ajili ya ndoto zetu, lazima siku tukiondoka
tuniani tuache alama.
Mwandishi wa kitabu hiki
amenitafakarisha sana aliposema, huwa tukifa wanasema, รpumzike kwa
amani,” anaendelea kusema kwamba “Kuna watu hawasitaili kuambiwa
ampumzike kwa amani maana muda wao mwingi hapa duniani ulikuwa wa
kupumzika”.
Amka sasa usibweteke anza kuzifanyia kazi
ndoto zako. Kumbuka kwamba watu wote waliofikia ndoto kubwa hawakuanzia
pakubwa walianzia padogo. Kuna aliyewahi kusema, “Kinachoanzia juu ni
kaburi tu”, hata kama vitu fulani havijakamilika wewe anza tu.
Kwenye
safari ya kuifikia ndoto yako au kuzifikia ndoto zako lazima ukumbane
na vigingi, lakini kumbuka hakuna ushindi bila mapambano lazima
uyashiriki mapambano hayo.
Kila hatua mpya inahitaji wewe mpya na mbinu mpya lazima uwe umejipanga.
Inawezekana
umekua ukisaidia kutimiza ndoto za wengine, sasa ni wakati wako kuamka
na kuanza kufanyia kazi ndoto zako, unaanzaje kuzifanyia kazi ndoto
hizo, mwongozo ulio katika kitabu hiki ni dira tosha iliyosheheni madini
na ramani ya kukupeleka kule unakotaka kufika na hata zaidi.
Nafikiri
kitabu hiki ni kitabu bora zaidi kukisoma katika vitabu vya Kiswahili
nilivyowahi kusoma kuhusu nama ya kuzifikia ndoto zangu, kimenijenga
sana na nimepata vitu vingi vipya ambavyo kweli sikuvifahamu.
Mwandishi
wa kitabu hiki, Godius Rweyongeza ni mtu ambaye nimemfahamu na
kumfuatilia kwa muda mrefu, mambo mengi anayoyaandika ni yale ambayo
tayari anayafanyia kazi na yameleta matokeo hivyo ukifuata kile
alichoandika ndugu Godius hautaacha kufika mbali sana.
Nikusihi
ukisome kitabu hiki si mara moja bali mara nyingi uwezavyo kwani madini
yaliyo humu ni lulu tosha ya kukuvusha wewe katika hatua uliyopo na
ukafika katika hatua zingine.
Pia maneno unayoyasoma
humu yaweke katika matendo, kuwa na vitu vingi kichwani bila kuviweka
katika matendo ni sawa na kuwasha gari bila kuliondoa, haufiki kokote.
Ukitaka kufika mbali fanya kwa matendo.
Mwisho wa yote
kumbuka, dunia inawapokea kwa mikono miwili wale wanaofanya mambo katika
matendo na kwa ubora wa hali ya juu, kwa msingi huo naunga hoja ya
Ralph Waldo Emerson aliyewahi kusema, “Kama mtu akiandika kitabu kizuri,
akahubiri mahubiri mazuri, au akatengeneza mtego wa panya mzuri kuliko
jirani yake, hata akijenga nyumba yake msituni, dunia nzima itatengeneza
njia hadi mlangoni kwake.”
Utumie muda wako vizuri
maana kila kitu ni zao la muda. Vitu vyote vizuri unavyoviona
vilitengenezwa ndani ya muda fulani. Tumia muda wako kujiendeleza na
kujifunza kuhusu mambo yanayohusu ndoto zako, tumia muda wako kwa
wengine na mwisho tumia muda wako kutengeneza huduma au bidhaa fulani.
Hivi ndivyo watu wote wenye ndoto kubwa walivyofanya na kufikia hatua za
juu.
Nampongeza sana na tena sana ndugu Godius
Rweyongeza kwa kitabu hiki kizuri kinachoelimisha, hamasisha,
tafakarisha lakini pia kinaburudisha kupitia stori mbalimbali
alizotuwekea humu.
*Ukianza kusoma kitabu hiki hutokichoka!*
Ndimi,
Edius Katamugora (Kijana wa Maarifa)
Mwandishi kitabu cha Yusufu Nina Ndoto.
Rafiki
yangu, bila shaka umeona aliyosema Edius Katamugora. Binafsi sima Cha
kuongeza labda kukwambia tu kuwa sasa ni zamu yako kupata kitabu hiki.
Nakala ngumu ya kitabu hiki ni elfu 20 tu.
Ukiihitaji soft copy ya kitabu hiki pia inapatikana pamoja na vitabu vingine Viwili kwa elfu 19,999.
Karibu Sana. Tuwasiliane kwa 0755848391 karibu